Ijumaa , 18th Feb , 2022

Nyota wa Manchester united Cristiano Ronaldo na Harry Maguire wako katika hali ya mvutano wa kuwania unahodha wa Manchester United huku kocha wa muda wa kalbu hiyo Ralf Rangnick akifanya mazungumzo na nyota hao wawili.

(Harry Maguire na Cristiano Ranaldo wakijadili jambo kwenye mechi.)

Ripoti inaeleza kuwa lengo la koch huyo kuongea na wachezaji hao ni kuhusu kufikia muafaka wa kufanya mabadiliko ya Ronaldo kuchukua kitambaa cha unahodha kwa muda uliobaki hadi msimu huu utakapo malizika.

Kwa mujibu wa chanzi cha taarifa hii inasemekana kuna imani inayoongezeka ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji wa united kwamba Ronaldo anastahili kuchukua nafasi ya nahodha, Ingawa wazo hili linampa shinikizo Maguire, ambaye bado anasita kukubaliana na kuachia nafasi hiyo sababu hataki kuipoteza kabisa nafasi hiyo, huku bado akihangaika kuwa na kiwango bora kwa nafasi yake ya mlinzi wa kati.

(Harry Maguire na Cristiano Ronaldo wakiwa mazoezini.)

Hapo awali Ronaldo alikuwa akiwahimiza wachezaji wenzake kumuunga mkono Maguire, Lakini tatizo ni kocha Ralf Rangnick anataka Ronaldo awaongoze wachezaji wote wadogo. Maana Ronaldo ndio amekuwa akiwashauri wachezaji wachanga tangu Rangnick alipowasili mwezi Novemba mwaka jana hivyo yeye ndio anastahili kuwa kiongozi.